Waziri Dkt.Kijaji achaguliwa kuwa Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa AfCFTA

DAR ES SALAAM-Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA Council of Ministers) kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Desemba 7, 2023.
Aidha, Waziri Kijaji ameongoza Mkutano wa 12 wa Baraza la Mawaziri wa Eneo Huru la Biashara Afrika Desemba 7, 2023 ulioanza Desemba 6, 2023 sambamba na Kongamano la Pili la AfCFTA la Wanawake katika Biashara lililoanza Desemba 6, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo chini ya Uenyekiti wa Waziri Dkt.Kijaji umepitisha Itifaki ya AfCFTA ya Wanawake na Vijana katika Biashara ambayo imekamilika chini ya usimamizi wa Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri na Muungano wa Tanzania na Mhamasishaji Mkuu na Kinara wa Wanawake na Vijana katika Biashara Barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news