Waziri Mhagama ashiriki maziko ya aliyekuwa Diwani wa Mbinga Mhalule

RUVUMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika Sera, Bunge na Uratibu ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama ameshiriki katika maziko ya marehemu Nasri Nyoni aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mbinga Mhalule Iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) (Mb.) Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama na Mbunge wa Madaba, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Mbinga Mhalule marehemu Nasri Nyoni.

Katika ibada hiyo mazishi iliyofanyika katika Kijiji cha Matomondo Waziri Mhagama ametoa pole kwa Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Songea Vijijjni na wafiwa wote.

“Mimi kama Mbunge na Diwani nimepoteza Mwenzangu Marehemu, Nasri alikuwa rafiki yangu kikazi, na tumeshirikiana sana kuleta maendeleo katika kata hii na nyinyi wananchi ni mashahidi tukisimamiwa na ilani ya Chama Cha Mapinduzi,”alibainisha.

"Naomba niwahakikishie Wanambinga Mhalule mnao ushirikiano wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, wote wako pamoja wako na nyie."

Aliendelea kusema kuwa, Serikali itaendelea kuhakikisha Mbinga Mhalule inaendelea kusonga mbele kama alivyokuwa anasimamia aliyekuwa Diwani wa mbinga Mhalule, ili kuendelea kumuenzi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Ndg. Odo Mwisho amesema jambo kubwa ni kuendelea kufarijiana na kuendelea kumuombea Mwenzetu aliyetutangulia.

“Amefanya mambo mengi wa kushirikiana na wananchi na sisi tumeona, tunamatarajio makubwa sana kwamba katika haya maisha ambayo ameyaanza ataenda kupata utukufu,” alifafanua Mwenyekiti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news