WIZARA YA ARDHI KUFANYA TATHMINI HALI YA MAAFA HANANG'

MANYARA-Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Mhandisi Anthony Sanga amewasili katika Kijiji cha Gendabi Wilaya ya Hanang' pamoja na wataalamu ya Wizara kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya maafa yaliyoasababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha Nchini kote.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhandisi Anthony Sanga pamoja na Mthamini Mkuu wa Serikal, Evelyne Mugasha wakiwa na Mkuu wa Operesheni ya Uokoaji kutoka Jeshi la Zimamoto, Kamishna Mbaraka Semwanza ambaye pia ni Mkuu wa operation ya maokozi wakikagua eneo la Kijiji cha Gendabi lililoathiriwa na mvua kwa lengo la kufanya uhakiki wa hali ya maafa.

Aidha,Mhandisi Sanga ameunda timu ya Wataalamu mbalimbali itakayofanya kazi ya tathmini ya maafa hayo kufuatia maporomoko ya magogo,mawe na matope yaliyosababishwa na mvua, zinazoendelea kunyesha hapa nchini.

Pamoja na mambo mengine timu hiyo ya wataalamu itafanya tathimini ya kiwango cha uharibifu wa mali,makazi na Shughuli za wananchi.

Hatua hii ya Katibu Mkuu Sanga kutekeleza maagizo ya haya Waziri Mkuu ya kuitaka serikali kufanya tathmini ya hali maafa ili wananchi waliokumbwa na maafa waweze kutokana na madhara yaliyosababishwa mafuriko hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news