Harambee ya Prof.Muhongo yafanikisha upauaji wa madarasa ya Shule Shikizi Kiunda

NA FRESHA KINASA

MBUNBE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo ameendesha harambee iliyolenga kukamilisha kazi ya upauaji wa boma la Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende jimboni humo.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Januari 16, 2024. Ambapo harambee hiyo imefanyika Januari 12, 2024.

Boma hilo ni la vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu. Boma limejengwa kwa michango ya Wana-Kitongoji cha Kiunda, Diwani wa Kata na Mbunge wa Jimbo hilo.
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374 ina shule za msingi zenye idadi 111 shule za Serikali, 4 shule Binafsi na 12 shule shikizi zinazopanuliwa.

Taarifa hiyo imesema kuwa harambee ya Shule Shikizi Kiunda Gharama zote za upauaji ni Shilingi 4,268,000.
FEDHA ZILIZOPATIKANA KWENYE HARAMBEE Tsh. 1,285,000.

Wachangiaji:

(i) Wakazi wa Kijiji cha Kamguruki

(ii) Wakazi kutoka Vijiji jirani

(iii) DEO Hamisi Shemahonge

(iv) Viongozi wa Chama Wilaya & Jumuiya zake ambao ni Ndg Jackson Nyakia, Ndg William Magero, Ndg Bwire Mkuku na Ndg Sophia Maregesi

Mabati yaliyopatikana kwenye Harambee:

(i) Ndg Pascal Maganga: Mabati 24

(ii) Diwani Mhe Kisha Marere: Mabati 36

(iii) Mbunge Prof Muhongo: Mabati 72

Ratiba ya upauaji
Tarehe 23.2.2024

Mbao za paa (kenji) zianze kuwekwa
Tarehe 24.2.2024

Mabati yaanze kuwekwa (kuezeka)

Kaimu Mtendaji wa Kijiji (VEO), Ndg Magreth Malima anapewa pongezi nyingi za usimamiaji mzuri wa shughuli za maendeleo ndani ya Kijiji cha Kamguruki.

MICHANGO INAKARIBISHWA SANA

Wana-Kitongoji cha Kiunda, na Kata ya Nyakatende kwa ujumla wanaendelea kuomba michango kutoka vyanzo mbalimbali ili kujenga na kupanua Shule Shikizi Kiunda iwe Shule ya Msingi kamili, inayojitegemea.

Tuma mchango wako wa fedha kwenye Akaunti ya Kijiji cha Kamguruki;

Akaunti ya Benki:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300679

Jina la Akaunti: Kijiji cha Kamguruki

Picha juu zikionesha wakazi wa Kitongoji cha Kiunda na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Harambee iliyofanyika kwenye eneo la ujenzi wa Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende, Musoma Vijijini. Tuendelee kuboresha miundombinu ya elimu ya Musoma Vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news