Kawe walia na ukabaji, uyang'anyi majira ya jioni

DAR ES SALAAM-Wakazi wa Kawe katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam, wameliomba Jeshi la Polisi nchini kuongeza ulinzi hasa nyakati za jioni eneo la Tanganyika Packers kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukabaji na unyang'anyi kwa kutumia silaha hususani za jadi.
Ni uhalifu ambao unadaiwa kufanywa na vijana wanajitambulisha kama Ulinzi Shirikishi kabla ya kumuibia mhusika.

Wamedai kuwa, ukikutana na vijana hao hujitambusha kama watu wa usalama na baada ya hapo hutekeleza uovu huo kwa kutoa mapanga,visu,nondo na kumuibia muhusika.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi wa Kawe ambao wawili walikataa kutotajwa kwa majina, wamedai kuwa kumekuwepo kwa vitendo hivyo katika eneo hilo ambalo ni karibu zaidi na Kituo cha Polisi Kawe.

Wamedai hivi karibuni mmoja wa Askari wa Jeshi anadaiwa kukabwa akiwa na mpenzi wake katika eneo hilo, jambo ambalo linaongeza wasiwasi miongoni mwao.

Williams Nashoni ni mmoja wa mkazi wa maeneo hayo amesema kuwa, kumekuwepo kwa vitendo hivyo kwa kiasi kubwa japo hivi karibuni vimepungua kutokana na baadhi ya walinzi wa Mtume Mwamposa kuongeza ulinzi,hata hivyo alidai bado jitihada zinatakiwa kuongezwa kutokana na walinzi hao kutokidhi mahitaji.

Nashoni amesema, kinachowaumiza ni vitendo hivyo kutokea eneo ambalo si mbali na kituo cha Polisi Kawe huku akiwaomba wahusika kujitathimini.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Mtatiro Kitinkwi amesema kuwa, wamejipanga kuendeleza kudumisha ulinzi na usalama eneo nzima la mkoa wa kipolisi ikiwemo Kawe na Tanganyika Packers.

Amesema kuwa, taarifa zote za uhalifu wanazipokea na watahakikisha wanazifanyia kazi ili kuhakikisha ulinzi na usalama kwa raia unaimarika zaidi.

Pia, amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa zote za uhalifu katika mkoa huo ili kuwarahisishia kazi na kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news