Musoma Vijijini kufanya kikao cha kugawa vifaa vya ujenzi kupitia Mfuko wa Jimbo

NA FRESHA KINASA

JIMBO la Musoma Vijijini mkoani Mara chini ya Prof. Sospeter Muhongo linatarajia kufanya kikao cha kugawa vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo.
Ni utaratibu wa Jimbo la Musoma Vijijini kufanya hivyo chini ya Mbunge wake Mheshimiwa Prof. Muhongo ambapo fedha za mfuko huo zimekuwa zikipelekwa kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo na miradi katika kuhakikisha zinawaletea maendeleo wananchi jimboni humo.

Kikao kitafanyika Januari 4, 2024 majira ya saa nne asubuhi katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma zilizopo Kijiji cha Suguti.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini leo Januari 2, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, washiriki ni Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo na waliotuma maombi mwakilishi mmoja tu. imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news