Makamu wa Rais Dkt.Mpango awasili Uswisi kushiriki Mkutano wa WEF

DAVOS-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango leo Januari 14,2024 amewasili nchini Uswisi ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) utakaofanyika Januari 15 hadi 19, 2024 katika mji wa Davos.
Katika Mkutano huo, Makamu wa Rais atahudhuria mikutano mbalimbali inayohusu masuala ya uchumi na uwekezaji, utawala bora, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kilimo.

Aidha, Mheshimiwa Makamu wa Rais atafanya mazungumzo ya uwili na viongozi wa mataifa na mashirika mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa hayo.
Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi na Makampuni mbalimbali duniani pamoja na Wafanyabiashara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news