Mtenga amshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuiheshimisha Mtwara Mjini kwa maendeleo

MTWARA- Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini mkoani Mtwara,Mheshimiwa Hassan Mtenga ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwaheshimisha wana Mtwara Mjini kupitia miradi ya maendeleo.

"Kwa niaba ya wapiga kura wa Jimbo la Mtwara Mjini kabla hatujaingia kwenye mwaka mpya 2024, maeneo mengi niliyopita wananchi walikuwa wananieleza tupelekee salamu zetu za kumpongeza Rais wetu Dkt. Samia;
Mheshimiwa Mtenga ameyabainisha hayo mjini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea kuhusiana na miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.

Amesema, Serikali imetatatua changamoto mbalimbali ndani ya jimbo hilo ikiwemo miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, migogoro ya ardhi na Uwanja wa Ndege, hatua ambayo inampa nguvu ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa bidii zaidi.

Vile vile, Mheshimiwa Mtenga amepongeza utendaji kazi unaofanywa na Mkurungenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo, Mwalimu Hassan Nyange kutokana ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu aripoti katika manispaa hiyo amekuwa na usimamizi nzuri wa ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato kwenye manispaa hiyo.

“Toka naingia mimi kuwa Mbunge kwenye jimbo hili, hatujawahi sisi kwenye akaunti ya manispaa kuwa na hata milioni 60, hatujawahi toka 2020/21 mpaka hapa Nyange (Mkurugenzi wa Manispaa) anaingia,”amesema Mheshimiwa Mtenga.

Amesema, Mkurugenzi huyo wakati anaingia manispaa hiyo iliikuwa na shilingi milioni 5.757 kwenye akaunti yake, kabla ya makusanyo kuanza kuongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 1.5 zilizokusanywa kwa muda wa wiki tano.

"Manispaa yetu kulikuwa na shilingi milioni 5.757 tu, hela ya halmashauri, wiki ya pili Mkurugenzi akakusanya milioni 28, wiki ya pili hiyo, ilipoingia wiki ya tatu akakusanya milioni 129 ilipofika wiki ya nne akakusanya milioni 695, ilipoingia wiki ya tano akakusanya bilioni 1.5,"amesema Mtenga.

Kuhusu huduma ya maji, Mheshimiwa Mtenga amesema, ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma ya maji safi na salama wanakwenda kufanya maboresho makubwa ya mfumo wa maji hususani kuweka mabomba mapya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news