Musoma Vijijini waishukuru Serikali ya Awamu ya Sita

NA FRESHA KINASA

WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara wamesema wanaishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha huduma ya upatikanaji wa huduma ya maji Safi na Salama jimboni humo katika kuchochea maendeleo yao.
Mbali na kumpongeza Mheshimiwa Rais pia wamemshukuru Mbunge wa jimbo hilo, Prof. Sospeter Muhongo kwa kuwa nao bega kwa bega na kushirikiana na Serikali katika kufuatilia miradi ya maji na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Nyaonje Masatu ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Bukumi wilayani Musoma amesema kuwa, hivi sasa huduma ya maji safi na salama imezidi kuimarika katika kijiji hicho. Hivyo, wananchi hasa kina mama wamekuwa wakipata huduma hiyo karibu na makazi yao.

Amesema, hali hiyo inasaidia kina mama kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kumtua ndoo mama kichwani.

Thomas Elias Mwenyekiti wa Kijiji cha Wanyere amesema, kwa asilimia kubwa kina mama wanapata maji karibu na makazi yao hivyo dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kumtua mama ndoo kichwani imefanikiwa kwa asilimia kubwa chini ya usimamizi madhubuti wa mbunge Prof. Muhongo ambaye ni mpenda maendeleo na amekuwa mstari wa mbele kupigania maendeleo ya Wananchi wake.

Sadick Mwise ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Sugiti amempongeza Mheshimiwa Mheshimiwa Raid Dkt. Samia kwa kutoa fedha nyingi ambazo zimetekeleza miradi ya maji maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Vijiji vya Jimbo la Musoma Vijijini na kuwarahisishia Wananchi huduma ya maji Safi na salama.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt.Halfan Haule amesema, "Serikali yetu imetoa shilingi bilioni 4, tunatekeleza miradi mitano kwenye Halmashauri yetu, tuendelee kuisimamia inayotoa huduma iliyokusudiwa kwa Wananchi. Na itakayoanza tuwe bega kwa bega kuhakikisha tunaikamilisha,"amesema Dkt. Haule.

Kwa upande wake Mhandisi Chacha Mwise kutoka Ofisi ya RUWASA Wilaya ya Musoma amesema kuwa, upatikanaji wa Maji Safi na Salama kwa Sasa ni asilimia 73 na miradi sita ambayo wanaitekeleza ikiisha watafikia asilimia 86 na katika Bajeti ya mwaka 2024/2025 watafikia asilimia 93, na Wakilenga kufikia asilimia 85 ya upatikanaji wa Maji Vijijini kama ilivyo ilani ya chama cha Mapinduzi na wanaendelea na miradi ya Shilingi Bil. 2.9 ambazo zimetolewa na Serikali.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa ja Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Januari 17, 2024 imebainisha kuwa Vijiji vyote 68 vyaJimbo la Musoma Vijijini vinasambaziwa maji safi na salama ya bomba kutoka Ziwa Victoria.

"Miradi hiyo ya usambazaji maji ya bomba iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji. Usambazi maji ya bomba vijijini mwetu unafanywa na:

(i) RUWASA

(ii) MUWASA

(iii) Mradi wa Mugango-Kiabakari-Butiama," imeeleza taarifa hiyo

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news