Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt.Samia katika mkutano Uganda

KAMPALA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa amewasili leo Januari 18, 2024 nchini Uganda akimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali zisizofungamana na Upande wowote (NAM) ulioanza tarehe 15 - 20 Januari, 2024.
Pia, Mheshimiwa atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia katika mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+China utakaofanyika tarehe 21-22 Januari, 2024, Kampala-Uganda.

Ujumbe wa Waziri Mkuu katika Mikutano hiyo utajumuisha viongozi waandamizi wa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa January Makamba.

Mkutano wa NAM hufanyika kila baada ya miaka mitatu na Mkutano wa mwisho, wa 18 ulifanyika jijini Baku nchini Azerbaljan mwezi Oktoba, 2019. NAM ni umoja wa nchi na Serikali 120 zenye msimamo wa sera ya kutofungamana na upande wowote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news