Naibu Waziri Pinda ashiriki maziko ya mtumishi wa Wizara ya Ardhi

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM

NAIBU Waziŕi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geophrey Pinda ameshiriki katika maziko ya mtumishi wa Wizara ya Ardhi makao makuu, Joyce Shayo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Mhe. Geophrey Pinda, Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera pamoja na watumishi wa Wizara ya Ardhi wakiwa na familia ya marehemu Joyce Shayo wakati wa maziko yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geophrey Pinda akiaga mwili wa aliyekuwa mtumishi wa Wizara ya Ardhi Joyce Shayo wakati wa maziko yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe. Geophrey Pinda na Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera wakiwa na familia ya marehemu Joyce Shayo wakati wa maziko yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024.

Maziko hayo yaliyohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Lucy Kabyemera ambapo yamefanyika Januari 3, 2024 katika eneo la Uru mkoani Kilimanjaro.

Marehemu Joyce Shayo amefariki Desemba 30,2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar Es Salaam akisumbuliwa na shinikizo la damu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geophrey Pinda na Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera wakiweka shada la maua wakati wa maziko ya marehemu Joyce Shayo yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024.
Watumishi wa Wizara ya Ardhi wakiweka shada la maua wakati wa maziko ya marehemu Joyce Shayo yaliyofanyika Uru mkoani Kilimanjaro tarehe 3 Januari 2024.
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua wakati wa maziko ya mama yao, Joyce Shayo.
Wazazi wa marehemu, Joyce Shayo wakiweka shada la maua.
Sehemu ya waombolezaji katika msiba wa Joyce Shayo. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Marehemu atakumbukwa zaidi kwa kuwa sehemu ya timu ya wataalamu waliokuwa wakifanya kazi ya Utatuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji 975. Marehemu ameacha watoto watatu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news