NECTA yawafutia matokeo wanafunzi darasa la nne na kidato cha pili

NA GODFREY NNKO 

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kitaifa ya upimaji wa darasa la nne na kidato cha pili uliofanyika mwaka 2023.

NECTA imebainisha kuwa, ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.13 kwa kidato cha pili na asilimia 0.39 kwa darasa la nne.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed amesema, baraza hilo limefuta matokeo kwa wanafunzi 178 wa darasa la nne na 28 wa kidato cha pili waliofanya udanganyifu.


Aidha,baraza limewafutia matokeo wanafunzi watatu wa darasa la nne na 14 wa kidato cha pili walioandika matusi.

Dkt.Mohamed amesema, katika masomo ya darasa la nne, matokeo yanaonyesha ufaulu wa sayansi na teknolojia ukifikia asilimia 86.86 kutoka asilimia 83.19 ya mwaka 2022 na somo la hisabati likifiki asilimia 54.00 kutoka asilimia 49.7.


Vile vile kidato cha pili, ufaulu wa somo la uraia umeimarika kutoka asilimia 31.12 mwaka 2022 hadi kufiki asilimia 48.27.

Dkt.Mohamed amesema kuwa, matokeo ya darasa la nne, wanafunzi 1,287,934 sawa na asilimia 83.34 wamefaulu kuendelea na darasa la tano.

Aidha,kwa kidato cha pili, wanafunzi 592,741 ambao ni sawa na asilimia 85.31 wamefaulu kwa daraja la kwanza hadi la nne katika mtihani huo uliofanyika kati ya Oktoba na Novemba,2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news