Neema inakuja nyumba za wafanyakazi Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, kwa kipindi kifupi kijacho Serikali itaanza kuweka mawe ya msingi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika hospitali za wilaya ikiwemo Kinyasini ya Wilaya ya Wete,Vitongoji Wilaya ya Chakechake, Micheweni Wilaya ya Micheweni kwa upande wa Pemba.

Pia upande wa Unguja kwa Hospitali ya Kitogani Wilaya ya Kusini Unguja, Pongwe Wilaya ya Kati, Pangatupu Wilaya ya Kaskazini B na Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Januari 3, 2024 alipoweka Jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa nyumba za Wafanyakazi katika Hospitali ya Abdulla Mzee Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, matayarisho ya ujenzi wa nyumba hizo yameanza ili kuendeleza mafanikio ya sekta ya afya nchini kwa kuondoa tatizo la kukosekana kwa Daktari au wafanyakazi wengine wa sekta ya Afya wanapohitajika kutoa huduma katika hospitali hasa wakati wa dharura.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amefarijika kushuhudia kwa vitendo ahadi iliyotolewa na Serikali ya China kutimia kufanikisha mradi wa ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika Hospitali ya Abdulla Mzee.
Vile vile amesema, mradi huo utawapunguzia masafa wafanyakazi na kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni vipaumbele vya Serikali ilivyoelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news