Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na Mlandege FC katika hafla maalum Ikulu

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa shukrani kwa Kamati ya maandalizi ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi mwaka huu chini ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe.Hemed Suleiman Abdullah kwa uratibu mzuri.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo usiku wa kuamkia leo Januari 22,2024 alipojumuika na wachezaji, viongozi wa timu ya Mlandege katika hafla ya chakula cha usiku alichowaandaliwa Ikulu jijini Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza Kamati ya Mapinduzi Cup chini ya Mbarouk Suleiman Othman, pia amewashukuru wadhamini mbalimbali wa mashindano hayo.
Vile vile ameipongeza timu ya Mlandege kwa kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mara ya pili mfululizo.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amepokea ombi la timu ya Mlandege kuhakikisha wanapatiwa Jengo la Makao makuu ya klabu yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news