Red eyes yasambaa mikoa 17 nchini

DODOMA-Serikali kupitia Wizara ya Afya, imesema jumla ya mikoa 17 nchini imekumbwa na ugonjwa wa macho mekundu ujulikanao kitaalamu kama viral keratoconjunctivitis (red eyes) na watu 5,359 wametajwa kuathirika.

Aidha,kufuatia kusambaa huko, wizara imewaasa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo unaosababishwa na maambukizi ya kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho.

Takwimu hizo zimetajwa Januari 29, 2024 na Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Profesa Paschal Rugajjo alipokuwa akitoa taarifa kuhusu hali ya ugonjwa huo kwa sasa.

Amesema,hadi kufikia Ijumaa Januari 26, idadi ya waliofika kwenye vituo vya afya walifikia 5,359 kutoka wagonjwa 1,109 Januari 19,2024.

“Ugonjwa huu umesambaa zaidi ingawa ni wachache ndiyo wanafika vituo vya huduma za afya, mpaka sasa ugonjwa huu umesambaa na kuongezeka katika mikoa 17 ikiwemo ya Singida, Katavi, Kilimanjaro, Mara, Iringa, Njombe, Ruvuma, Simiyu, Mtwara, Lindi, Songwe, Rukwa na Mwanza,” amesema.

Amesema, awali ugonjwa huo ulikuwepo katika mikoa minne ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Pwani.

Vile vile, amesisitiza suala la usafi ni jambo muhimu katika kuzuia maambukizi kusambaa kwa wengine Kutokana na tabia ya ugonjwa huu kusambaa kwa kasi, maambukizi haya huleta mlipuko ambao husambaa kupitia kirusi kwa asilimia zaidi ya asilimia 80.

Prof.Ruggajo amewashauri wananchi kutokutumia dawa zisizo rasmi na ambazo hazijaandikwa na daktari kwa wakati huo na kutotumia dawa za macho anazotumia mgonjwa mwingine ili kuepuka madhara kwa kuwa dawa za macho ni tofauti na kwa matumizi tofauti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news