Salamu za Mwaka Mpya 2024 kutoka kwa Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi anawatakia Heri ya Mwaka Mpya 2024 wananchi wote na kuwataka kudumisha umoja, amani na upendo waliouonesha katika mwaka 2023.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi anasema kuwa, mwaka 2023 ulikuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwa Wazanzibari katika sekta mbalimbali kama vile Elimu, Afya, Miundombinu, Uwezeshaji na mengineyo, mwaka mpya 2024 utakuwa wa mafanikio zaidi kulingana na mipango ambayo Serikali imejipanga kuitekeleza kwa wakati.

Aidha,Mhe. Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa watumishi wa umma kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia msingi ya Sheria na Weledi ili Zanzibar iendelee kupiga hatua za mafanikio.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news