Simba SC yatinga fainali Mapinduzi CUP

ZANZIBAR- Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imetinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 3-2 dhidi ya Singida Fountain Gate.
Ni kupitia mtanange wa nguvu ambao umepigwa leo Januari 10,2023 katika Uwanja wa New Amaan Complex jijini Zanzíbar.

Licha ya Singida Fountain Gate kutangulia kwa bao la mshambuliaji Elvis Rupia dakika ya 11 mambo hayakuwa kama walivyopanga.

Kwani,Fabrica Luamba Ngoma aliwasawazishia waajiri wake bao hilo dakika ya 90+ ya mchezo huo.

Wawili hao kutoka Tanzania Bara walimaliza vipindi vyote wakiwa sare ya bao moja kwa moja ndipo ikachezwa mikwaju ya penalti.

Kupitia mikwaju hiyo kipa wa Simba SC, Ali Salim ameokoa penalti za mabeki Gardiel Michael, Hamad Waziri na mshambuliaji Meddie Kagere kuipa Simba tiketi ya Fainali Kombe la Mapinduzi.

Aidha,waliofunga penalti za Simba SC ni viungo Luis Jose Miquissone,Israel Patrick Mwenda na Moses Phiri huku ya Shomari Kapombe ikiokolewa.

Vile vile, penalti ya na Saido Ntibanzokiza imegonga mwamba wa juu na kwenda nje. SFG waliofunga ni Abuya na Deus Kaseke.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news