Sudan yamrejesha nyumbani Balozi wake nchini Kenya

KHARTOUM-Sekali ya Jamhuri ya Sudan imemuita nyumbani balozi wake nchini Jamhuri ya Kenya,Kamal Jubbara ikipinga hatua ya Rais Dkt.William Ruto ya kufanya mazungumzo na kamanda wa wanamgambo wa RSF, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.
Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt.William Ruto akiwa na Kiongozi wa RSF, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo katika Ikulu ya jijini Nairobi tarehe 3 Januari, 2024. (Picha na PCS).

Kwenye taarifa iliyorushwa na shirika rasmi la habari la SUNA, kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan,Ali al-Sadiq amesema, balozi huyo amerejeshwa nyumbani kwa mashauriano ya kupinga mapokezi rasmi yaliyoandaliwa na serikali ya Kenya kwa ajili ya kiongozi huyo wa wanamgambo.

Amesema, mashauriano hayo yataangazia uwezekano wa namna hatua hiyo inavyoweza kuathiri uhusiano kati ya Kenya na Sudan.

Dagalo, ambaye vikosi vyake vinapambana na jeshi la Sudan linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan amekua ziarani katika baadhi ya mataifa ya Afrika ambayo ni pamoja na Uganda, Ethiopia na Djibouti, Kenya na sasa yuko Afrika Kusini.

Uhusiano baina ya Burhan na serikali ya Kenya umekuwa katika mvutano kwa miezi kadhaa, wakati Nairobi ikiangazia kuendeleza mawasiliano na Daglo ili kusuluhisha mzozo baina ya majeshi hayo mawili ya Sudan.

Katika hotuba yake ya Januari 1, Jenerali Burhan alionya kwamba serikali za Afrika zinazoandaa ziara za "wauaji hao" "zinajionyesha dhahiri kuwa ni washirika katika mauaji ya watu wa Sudan".

Juhudi za upatanishi kwa kiasi kikubwa zimesimama katikati ya ongezeko la uadui kati ya majenerali hao wawili.

Vita hivyo vimesabaisha vifo vya zaidi ya watu 12,000, hii ikiwa ni kulingana na makisio ya taasisi ya Armed Conlfict Location and Dat Event Project, huku zaidi ya watu milioni 7 wakilazimika kuyakimbia makazi yao, umesema Umoja wa Mataifa (DW)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news