TFF yamsimamisha kazi Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche

DAR ES SALAAM-Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemsimamisha kazi, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mualgeria Adel Amrouche na kumteua, Hemed Suleiman (Morocco) kuwa, Kaimu Kocha Mkuu.
Hayo yanajiri baada ya Shirikisho la Soka barani Afrika kumfungia mechi nane Amrouche kwa kutoa kauli zisizo za kiungwana dhidi ya Morocco.

Ni kuelekea mchezo wa kwanza wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko nchini Ivory Coast.

Amrouche ameituhumu Morocco kuwa inajipangia muda wa kucheza mechi zake na marefa wa kuchezesha pia akilenga kuaminisha ni kwa sababu hiyo wanafanya vizuri.

Simba wa Atlasi, Morocco wailifunga Tanzania, Taifa Stars 3-0 kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa Kundi F Jumatano Uwanja wa Laurent Pokou jijini San-Pedro nchini Ivory Coast.

Mabao ya Simba wa Atlasi yalifungwa na beki wa Al-Shabab ya Saudí Arabia, Romain Ghanem Paul Saïss dakika ya 30, kiungo wa Marseille ya Ufaransa, Azzedine Ounahi na mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Youssef En-Nesyri dakika ya 80.

Taifa Stars ilimaliza pungufu baada ya kiungo wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine, Novatus Dismas Miroshi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kuoneshwa kadi ya pili ya njano.
Taifa Stars inatarajiwa kuteremka tena Uwanja wa Uwanja wa Laurent Pokou jijini San-Pedro Jumapili Saa 2:00 usiku kumenyana na Zambia katika mchezo wa pili wa Kundi F, siku ambayo Morocco itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Saa 11:00 Jioni hapo hapo Uwanja wa Laurent Pokou.

Aidha,Morocco inaongoza Kundi F kwa alama zake tatu, ikifuatiwa na DRC na Zambia zenye alama moja kila moja, wakati Tanzania inashika mkia ikiwa na alama sifuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news