TOST kuwasuluhisha walipakodi na TRA

NA FARIDA RAMADHANI WF

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameiagiza Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) kuhakikisha inatatua migogoro mbalimbali ya kodi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kukusanya mapato pamoja na kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kushoto), akimkabidhi mwongozo wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438 kwa Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama, baada ya kuzindua Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Tax Ombudsman Service Tanzania - TOST), katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ni chombo huru chenye jukumu la kupitia na kushughulikia malalamiko yote ya walipakodi kuhusu huduma, masuala ya kiutaratibu na kiutawala yanayoweza kujitokeza katika usimamizi wa sheria za kodi zinazotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA.

Dkt. Nchemba alitoa agizo hilo Jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Ofisi hiyo mpya ambayo iko chini ya Wizara ya Fedha.

Mhe. Nchemba alisema kuwa Serikali inatarajia kwamba Ofisi hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya kikodi na kuongeza kiwango cha ulipaji kodi kwa hiari, hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

“Ofisi hii utasaidie kupunguza migogoro ya kodi na kuongeza kiwango cha ulipaji kodi kwa hiari, siku tukifanikiwa kuongeza idadi ya walipakodi (taxbase), tutakuwa na uhuru mkubwa sana wa kupunguza hivi viwango vya ulipaji kodi”, alisema Mhe. Dkt. Nchemba.

Alisema ni matarajio ya Serikali kuwa ustawi wa biashara utaongezeka kutokana na walipa kodi kupata jukwaa huru litakalotoa fursa ya kusikiliza changamoto zinazohusu usimamizi wa sheria ya kodi pamoja na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiitambulisha rasmi Tovuti ya Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Tax Ombudsman Service Tanzania – TOST-www.tos.go.tz), wakati wa Uzinduzi rasmi wa Taasisi hiyo katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali, Viongozi wa Wizara ya Fedha, Viongozi wa Dini, Taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na wanahabari.

Mhe. Dkt.Nchemba alisema Wizara ya Fedha itaendelea kusimamia na kuboresha utendaji wa Taasisi hiyo kwa kuhakikisha kuwa mahitaji yote muhimu yanapatikana ikiwemo rasilimali watu, vifaa na mifumo ya kisasa ili iweze kutoa huduma bora kwa walipa kodi.

Aidha, Aliagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kukusanya kodi kwa weledi kwa kutafuta njia ya majadiliano na wafanyabiashara wanaokiuka taratibu badala ya kufunga biashara zao.

Mhe. Dkt. Nchemba aliwaagiza Wafanayabiashara kufanya biashara zao kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni zilizopo ili kuepusha misuguano isiyo ya lazima na Mamlaka ya Mapato.

Pia alitoa rai kwa wananchi kuwa wazalendo kwa kulipa kodi stahiki na kwa wakati, kudai risiti halali kulingana na kiwango cha fedha walichotoa na wafanyabiashara kufanya matumizi sahihi ya mshine za kutolea risiti kwa njia ya kielekroniki (EFDs) pamoja na kutoa risti halali kwa wateja wao.

“Watu wanaostahili kutumia mashine za EFDs watumie, kutokufanya hivyo ni kujitafutia matatizo wenyewe. Kutokutoa risiti na kusingizia mifumo sio suluhisho la kudumu, huku ni kuahirisha matatizo” alisitiza Mhe. Dkt. Nchemba.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha Taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi - Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akibofya kuonesha Nembo rasmi ya taasisi hiyo kama ishara ya kuzindua Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi - Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama, akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi - Tax Ombudsman Service Tanzania”.

Alisema kufanya hivyo, kutaiwezesha Serikali kutoa huduma muhimu za kijamii ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayoboresha maisha yao na kupunguza umasikini ikiwemo maji, elimu, miundombinu wezeshi kiuchumi na mambo mengine mengi

Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya Usuhulishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST), Bw. Robert Manyama alisema kuwa Taasisi yake imejipanga kutatua changamoto za taarifa za kikodi za wananchi katika ubora wa hali ya juu kwa kuwa imeweka mazingira rafiki na rahisi ya wananchi kuwasilisha malalamiko yao popote walipo pamoja na kuwa na wafanyakazi wenye ueledi na waliotayari kutoa huduma kwa walipa kodi.

“Kipaumbele cha Ofisi hii ni kuhakikisha kwamba malalamiko yote yanashughulikiwa kwa uhuru kamili, haraka, haki na usawa”, alibainisha.

Alisema Ofisi hiyo imeanzishwa kutokana na marekebisho ya Sheria ya Fedha namba 8 ya mwaka 2019, yaliyosababisha marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi SURA 438, kwa kuongeza sehemu ya IIIA – Uanzishaji wa Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Establishment of Tax Ombudsman office.)

Bw. Manyama alisema marekebisho ya sheria yaliipatia Ofisi hiyo jukumu mahususi la kupokea, kusajili na kusuluhisha Malalamiko yatokanayo na usimamizi wa sheria za kodi ili kuyapunguza na kutoa mapendekezo ya maboresho ya mfumo wa ukusanyaji kodi nchini pamoja na kuongeza ulipaji kodi wa hiari na kupunguza gharama za ukusanyaji wa kodi ya Serikali.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb), alisema Kamati hiyo imependekeza Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi kuhakikisha inajulikana kwa wadau wote wa kodi nchini na itekeleze majukumu yake kikamilifu ya kutatua changamoto za walipakodi.
Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama, akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi - Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha Taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi - Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha Taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi - Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Viongozi mbalimbali wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, wakifuatilia kwa umakini halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi - Tax Ombudsman Service Tanzania”.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(katikati walioketi), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Bw. Daniel Sillo (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa kwanza kushoto walioketi), Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Frank Haule (wa pili kushoto walioketi) na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama (wa kwanza kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, baada ya kumalizika kwa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo, uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati walioketi), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Bw. Daniel Sillo (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa kwanza kushoto walioketi), Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Frank Haule (wa pili kushoto walioketi) na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama (wa kwanza kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, baada ya kumalizia kwa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati walioketi), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Bw. Daniel Sillo (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa kwanza kushoto walioketi), Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Frank Haule (wa pili kushoto walioketi) na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama (wa kwanza kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha, baada ya kumalizia kwa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Alisema,kamati pia imependekeza Ofisi hiyo kuendelea kushauri namna ya kutatua changamo ya mifumo ya kodi nchini iliyosababisha migogoro na kuifanyia marekebisho mifumo husika.

Mhe. Sillo aliishauri Ofisi hiyo iendelee kufanyia kazi changamoto za kikodi zinazojirudia na kutafuta suluhisho la kudumu huku akitolea mfano wa tatizo la utoaji na uombaji risiti.

Aidha, Kamati ilipendekeza Serikali, kupitia Taasisi hiyo, itafute mfumo wa kielektroniki utakaotumika kupokea malalamiko, kuyashughulikia na kutoa mrejesho huku kwa wadau na kusisitiza kuwepo uwazi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news