Wito wa kushiriki Kongamano kuhusu Maboresho ya Sera mpya ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001

DODOMA-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepanga kufanya Kongamano la Wadau kuhusu maboresho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 na Mkakati wake wa Utekelezaji, litakalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 9 Januari, 2024 kuanzia saa 3.00 asubuhi.

Lengo la Kongamano hilo ni kupata maoni ya wadau katika maeneo mapya yanayopendekezwa katika Sera ya Mambo ya Nje inayofanyiwa maboresho na pia maeneo mengine yaliyopo ambayo yanaendelea kutekelezwa kama yalivyokuwa katika Sera ya Sasa.

Kwa msingi huo, Wizara inaawalika wadau wote ikiwa ni pamoja na; Wanachuo/Wasomi, Wanasiasa, Vyama vya Siasa, Taasisi za Kidini, Asasi za Kiraia, Taasisi Zisizo za Kiserikali (NGOs) na wananchi kwa ujumla kushiriki Kongamano hilo muhimu litakalosaidia kukusanya maoni yatakayowezesha kupata Sera imara ya Mambo ya Nje.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news