ZMBF yaishukuru China

ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF),Mhe.Mama Mariam Mwinyi amekutana na Balozi mdogo wa China Mhe. Zhang Zhisheng anayefanyia kazi zake Zanzibar kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi nchini.
Balozi huyo amefika katika ofisi za ZMBF Ikulu Migombani leo Januari 30,2024.

Mama Mariam Mwinyi amemshukuru Mhe.Balozi Zhang Zhisheng kwa kuwa mdau mkubwa wa ushirikiano kati ya ZMBF kwa misaada mbalimbali ya maendeleo.

Naye, Balozi Mhe.Zhang Zhisheng amesema China itaendelea kudumisha ushirikiano na ZMBF.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news