Bodi ya Wakurugenzi ya BoT yatembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha

ARUSHA-Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, imetembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa, Bw. Misaeli Musa.
Katika ziara hiyo, Gavana Tutuba ameelezea mikakati mbalimbali inayochukuliwa na BoT katika kukuza na kuimarisha sekta ya fedha nchini ili kusaidia ukuaji endelevu wa uchumi na taifa kwa ujumla.

Akitoa taarifa kuhusu mkoa wake, Katibu Tawala Bw. Musa, alieleza mafanikio ya Mkoa wa Arusha katika sekta ya utalii na kusema yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na filamu ya "The Royal Tour".
Amesema, mkoa huo umeongezeka umaarufu pamoja vivutio vilivyopo vya utalii. Pia, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya mkoa na BoT katika kukuza maendeleo na ustawi wa jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news