CUF yatoa pole kifo cha Lowassa


SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD NGOYAI LOWASSA:

CUF- Chama Cha Wananchi kimepokea kwa huzuni taarifa za kufariki kwa Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

CUF- Chama Cha Wananchi kinatoa pole kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, familia ya marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu mzito. 

Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampe Pumziko la Amani marehemu Lowassa na awape subira njema familia na ndugu wa marehemu wakati huu mgumu wa majonzi.

BWANA ALITOA NA AMETWAA. JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE , AMINA!

Prof. Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti Taifa
CUF- Chama Cha Wananchi
Februari 11, 2024

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news