Kwaresma ni wakati wa kutubu, kuamini injili-Padri Masanja

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa wakati wa Kwaresma ni wa kutubu na kuamini injili na kama ilivyoelezwa wakati wa Jumatano ya Majivu na pia dominika hii jambo hilo linaendelea kutiliwa mkazo na kupewa msukumo wa juu zaidi.
Hayo yamesemwa katika Jumapili ya Kwanza ya Kwaresma, Februari 18, 2024 katika Kanisa la Bikira Maria-Malkia wa Wamisionari , Parokia ya Malya- Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza na Padri Samson Masanja ambaye pia ndiye Paroko wa Parokia hii.

Padri Masanja alisema kuwa uovu unamkasilisha Mwenyeenzi Mungu na dhambi inamchukiza Mwenyezi Mungu na kama mwanadamu akifanya dhambi anaweza kukutwa na gharika la wakati wetu .

“Ndiyo maana tunaona ghariba linalotokea wakati huo kutokana naukaidi wa watu na watu kutokuwa tayari kumrudia Mwenyezi Mungu na kuhongoka.”

Inawezekana yatatokea magonjwa, yakatokea mapigano na vita na kimbunga, tukumbuke upendo wa Mungu ni wa Kibaba, hivyo tuyafuate yale aliyotuagiza. Mungu mara zote anasema halitoweza kutoka Gharika Kuu tena, huo ni upendo mkubwa na agano la Mwenyeenzi Mungu kwetu na agano lake ni la haki.

Padri Masanja alisema kuwa katika somo la pili Paulo Mtume anasema kuwa Kristo mwenyewe amekuja ili kuifuta dhambi na ili sisi sote tuwe wenye haki

“Kristo ambaye hakuwa na dhambi, alikubali kuivaa dhambi, ili sisi tulio wadhambi tuwe na haki, akawa tayari kuteshwa, akawa tayari kufa lakini akaibuka kuwa mshindi.”

Padri Masanja aliongeza kuwa huu ni wakati wa Kwaresma,

“Huu ni wakati wa kutafakari, ni wakati wa hija, ni wakati wa kurudi kwa Mwenyeenzi Mungu, mimi na wewe tuwekeze katika kipindi hiki na tujitathimini kwa yale tunayoyafanya kwa ukaidi na tusiyompendeza Mungu , ili turudi, ili tuyapokea malipo yake kama anavyoeleza Yohane Mbatizaji kuwa wakati umetimia na mpango wa Mungu u jirani, tubuni na kuamini injili .”

Misa hii pia iliambatana na nia na maombi kadhaa,

“Eee Mungu, uwepo wako unajitokeza kwa dalili ya wema, upole na upendo. Utujalie kuwakilimie wenzetu upole, wema na upendo. Eee Bwana-Twakuomba utusikie.”

Wakati wa matangazo ya misa hiyo, waamini walikumbushwa kuwa kila wakati wa Ibada ya Njia ya Msalaba inapomalizika, zoezi la kuyasafisha maeneo ya makaburi linafanyika, ikumbukwe kuwa hakuna Mkristo asiye na marehemu popote aishipo.

“Hauna ndugu yako katika eneo la kaburi, tambua umefiwa jirani au umefiwa na mwanajumuiya, hivyo fika kwa ajili ya kumsafishia huyu ndugu, jirani au mwanajumuiya mwenzako. naombeni tuzingatie hilo. Marehemu wote wanatuhusu, fanyeni usafi wa makaburi kwa wakati .

Tuzingatie ibada za Njia ya Msalaba zipo sita wakate huu wa Kwaresma hivyo siku za usafi wa makaburi ni sita , lakini siku ni tano maana ibada ya Njia ya Msalaba ya Mwisho ina mambo mengi. Eneo letu la makaburi ni kubwa tukifika waamini 13, siyo rahisi kulimaliza maana majani ni mengi, miti imekomaa, tufikeni kwa wakati na tuje na mapanga, majembe na mafyekeo.”

Hayo yalinadiwa katika misa hiyo na msomaji wa matangazo. Kwa utaratibu wa mazoea ya Wakristo wengi ,wakati karibu ya Pasaka huwa ni muda wa kusafisha makaburi ya wafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news