Madiwani Mbinga wapongezwa

NA SILVIA ERNEST

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbinga, Ndg. Joseph Mdaka amewapongeza madiwani wa Wilaya ya Mbinga kwa kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali katika maeneo yao.
Pongezi hizo zimetolewa Februari 4, 2024 katika maadhimisho ya miaka 47 ya chama cha mapinduzi yaliyofanyika Kiwilaya katika Kata ya Maguu Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
"Niwapongeze sana madiwani wote wa Wilaya ya Mbinga mnafanya kazi kubwa na inaonekana, endeleni kushirikiana na wataalam katika kuwaletea wananchi maendeleo,"amebainisha Mdaka.
Aidha,Mdaka amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule ili waweze kupata elimu, amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya elimu ili boresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Aziza Mangosongo amewataka wananchi wa Wilaya ya Mbinga kuhakikisha wanaimarisha amani katika maeneo yao hasa katika kipindi tarajiwa cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

"Amani ni msingi wa kuleta maendeleo katika nchi yetu sehemu yoyote isiyo na amani haina maendeleo, tuilinde amani yetu,"amesisitiza Mangosongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news