Maji ya bomba yaendelea kusambazwa Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

SERIKALI inaendelea na zoezi la usambazaji wa huduma ya maji safi na salama katika Jimbo la Musoma Vijijini ili kuhakikisha wananchi jimboni humo wanapata huduma hiyo kwa ufanisi katika kuchochea maendeleo yao na usatawi wao kijamii na kiuchumi.
Ambapo, wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo fedha za miradi ya maji ambapo wamesema hivi sasa huduma ya maji safi na salama imeendelea kuimarika kutokana na Serikali kuendelea kutekeleza miradi ya maji.

Wamesema,hatua hiyo inachagizwa na uongozi imara, makini na madhubuti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo anavyojitoa kufuatilia miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi hao moja kwa moja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini leo Februari 21,2024 imeeleza kuwa,"Serikali kwa kupitia RUWASA na MUWASA inaendelea kusambaza maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria kwenda vijijini mwetu.

"MUWASA imepewe jukumu la kusambaza maji ya bomba kwenye Kata zilizo jirani na Mji wa Musoma. Kata hizo ni Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu.

"RUWASA inaendelea kusambaza maji kwenye vijiji vyote 68 vya jimboni mwetu, vikiwemo vijiji vya kata nne zilizotajwa hapo juu (ushirikiano wa RUWASA & MUWASA kwa baadhi ya vijiji vya jimboni mwetu)," imeeleza taarifa hiyo.
Magongwa Majinge ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkirira ambapo amesema kuwa, Serikali imeendelea kufanya vizuri katika uimarishaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi jirani na makazi yao jambo ambalo limewapa neema wananchi.

"Kinamama ambao awali walitumia muda mwingi kutafuta maji na kushindwa kufanya kazi za maendeleo kwa sasa wanashiriki shughuli za maendeleo na uzalishaji kwani maji yamesogezwa karibu yao. 

"Pongezi kwa Rais wetu na Mbunge kwa kugusa maisha ya wananchi miradi ya maji imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi kwa ustawi wao na jimbo letu pia," amesema Majinge.

Naye Rhoda Joseph amesema, kuwa upatikanaji wa maji safi na salama jirani na makazi ya wananchi unachangia shughuli za uzalishaji kufanyika, badala ya wananchi kutumia muda mwingi kuwaza na kutafuta maji muda wao watautumia katika uzalishaji na hivyo kujikwamua kiuchumi.

"Tuendelee kuwaamini Viongozi wetu Rais Dkt. Samia na Prof. Muhongo Mbunge wetu, yaliyoahidiwa wakati wa kampeni kwamba maji yatakuwa ya uhakika tunaona miradi ya maji inazidi kutekelezwa, shule zimejengwa, Maabara za Sayansi zinajengwa, hospitali na vituo vya afya pia. 

"Haya ni mageuzi ambayo tulidhani labda yasingetokea lakini kwa macho yetu tunayaona Musoma Vijijni,"amesema John Bwire.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) NIcas Mugisha amesema,"upande wa Musoma vijijini tumefika Etaro, Busamba, Mumahare lakini sasa tumefika Mkirira tunaendelea Nyegina ambapo kazi hiyo ndani ya mwezi huu. Tunacho chanzo chetu kikubwa cha maji kinazalisha maji ya kutosha kabisa,"amesema na kuongeza kuwa.

"Upande wao ni suala la kusogeza mtandao tu sababu chujio lipo, mtandao mkubwa wa mabomba umeshalazwa kinachofanyika kwenda kwenye hivyo vijiji ni extension tu kwa hiyo watapata maji ambayo ni safi na salama kutoka chanzo cha uhakika Ziwa Victoria,"amesema Nicas.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news