Waziri Mkuu wa DRC,Jean-Michel Sama Lukonde ajiuzulu

KINSHASA-Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Mheshimiwa Jean-Michel Sama Lukonde amejiuzulu.
Rais Félix Tshisekedi akiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa DRC, Jean-Michel Sama Lukonde. (PICHA NA MTANDAO).

Lukonde aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Felix Tshisekedi siku nane baada ya kuidhinishwa kwa nafasi yake kama mbunge wa kitaifa.

Kiongozi huyo kwa sasa atahudumu bungeni katika nafasi ya ubunge.

Aidha,ofisi ya rais imesema ombi lake la kujiuzulu limekubaliwa ingawa rais ameiomba serikali ya Lukonde kuendelea kuyashughulikia masuala ya sasa hadi pale serikali mpya itakapoundwa.

Lukonde aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati yenye utajiri wa madini mnamo Februari 2021. Alikuwa na umri wa miaka 43 wakati huo.

Baada ya kuchaguliwa tena Desemba, Tshisekedi alimteua mwakilishi baada ya kuchaguliwa tena Desemba kubainisha muungano wa walio wengi ndani ya Bunge la Kitaifa kwa lengo la kuunda serikali yake ijayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news