Mifugo 3,000 yahamishwa kutoka Ngorongoro kwenda Msomera,ulinzi waimarishwa

ARUSHA-Kundi la mifungo mingine ipatayo 3,000 imehamishwa kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera huko Handeni mkoani Tanga ili kupisha shughuli za uhifadhi na utalii katika eneo hilo.
Eneo ambalo ni miongoni mwa maeneo ya maajabu ya Dunia huku Jeshi la Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo nchini kikiwahakikishia usalama wa mifugo hiyo.
Hayo yamesemwa alfajiri ya leo Februari 23,2024 na Kamanda wa Polisi wa kikosi hicho nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP Simon Pasua wakati akitoa taarifa ya namna ambavyo jeshi hilo lilivyoimarisha ulinzi wa mifugo ya wananchi waliohama kwa hiari yao kutoka katikaMamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera huko Handeni mkoani Tanga.
Kamanda Pasua amebainisha kuwa, mifugo hiyo 3,379 ambayo imehamishwa ni kutoka kaya themanini na mbili ambazo zina jumla watu 41 ambao tayari wamehama kwa hiari kutoka mamlaka hiyo.
SACP Pasua amewahakikishia wananchi ambao bado wanaendelea kujiandikisha kuhama kwa hiari yao kuwa, jeshi hilo limeimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi pamoja na mifugo yao katika Kijiji cha Msomera.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news