Musoma Vijijini waishukuru Serikali

NA FRESHA KINASA

KILELE cha sherehe za miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Musoma Vijijini zimefanyika, huku wananchi na wanachama wa chama hicho wakiishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha huduma mbalimbali ambazo zimeboresha maisha yao.
Sherehe hizo zimefanyika Februari 5, 2024 katika Kijiji cha Seka Kata ya Nyamrandirira na kuhudhuriwa na Wananchi Viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya wilaya, kata, Matawi na Katibu wa ÇCM Mkoa wa Mara, Ibrahim Mjanaheri Ibrahim aliyekuwa mgeni rasmi.

Nancy Justine nkazi wa Kata ya Seka amesema kuwa Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeimarisha upatikanaji wa huduma ya maji Safi na salama maeneo mbalimbali jimboni humo. Ambapo changamoto ya kina mama kutembea umbali mrefu kutafuta maji kwa sasa imetoweka wanapata maji karibu na makazi yao.

"Wanawake tumshukuru sana Dkt. Samia Hassan katika suala la maji jimboni mwetu amefanya kazi kubwa sana. 

"Zamani tulitumia muda mwingi kutafuta maji mitoni na kwenye visima ambayo maji yake Si safi wala salama, lakini kwa Sasa tunapata maji karibu yetu na pia muda ambao zamani ulikuwa ukipotea kwa sasa haupotei tunafanya kazi za uzalishaji badala ya kutafuta maji kutembea umbali mrefu," amesema Nancy.
Joseph Masatu amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imefanya vyema katika uimarishaji wa sekta ya afya jimboni humo kwa kujenga Zahanati, vituo vya afya na pia kukamilisha ujenzi wa Hospital ya Halmashauri hiyo iliyopo Suguti yenye hadhi ya Hospitali ya Wilaya. Ambapo wananchi wanapata huduma kwa urahisi na karibu yao.

"Nampongeza Prof. Muhongo na Serikali ya Awamu ya Sita kwa hakika tumeona mageuzi makubwa katika uimarishaji wa sekta ya elimu. Mbunge ameshiriki Sana harambee za kuchangia ujenzi wa Maabara za masomo ya Sayansi katika shule za Kata zetu, ili Watoto wasome kwa vitendo na hili limeendelea kufanikiwa," amesema Juma Shadrack na kuongeza kuwa.

"Pia serikali imekiwa ikitoa fedha nyingi baadhi ya kata zina shule mbili yapo majengo mazuri kabisa yamejengwa Serikali imefanya kweli, tutaendelea kushirikiana na Serikali na Mbunge wetu kuona kwamba maendeleo ya Musoma Vijijini yanazidi kuimarika zaidi," amesema Juma Shadrack.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Ibrahim Mjanaheri Ibrahim, amepongeza kazi kubwa za kuleta maendeleo zinazofanywa na Serikali na Mbunge Prof. Muhongo na hivyo amewataka Wananchi waendelee kushirikiana naye na pamoja na Viongozi wote jimboni humo.

Ameongeza kuwa,Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia Dkt. Samia Suluhu Hassan kimejipanga vyema kuhakikisha ifikapo mwaka 2025, changamoto zote za wananchi zitakuwa zimetatuliwa kwa asilimia 100 huku akisema na tayari majibu yapo kwani miradi mingi imetekelezwa ambayo inagusa moja kwa moja maisha ya Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news