Polisi,IHET waja na mifumo kudhibiti shule za udereva zisizokuwa na sifa nchini

NA ABEL PAUL
Tanpol

KATIKA kuhakikisha mifumo inaondoa changamoto na malalamiko kwa wananchi hususani katika shule za udereva ambazo hazijasajiliwa, Jeshi la Polisi na Taasisi ya Mitambo Mizito na Teknolojia IHET wamekuja na mfumo uitwao (DSRS) Driving School Registration System ambao Utazitambua shule ambazo zimesajiliwa kwa mujibu wa sheria.
Akifungua mafunzo ya mfumo wa DSRS leo Februari 19, 2024 Msimamizi Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Naibu Kamishna wa Polisi,DCP Frasser Kashai amekipongeza chuo cha Ufundi Arusha na kikosi cha usalama barabarani kwa namna walivyobuni njia sahihi ya kuja na mfumo wa usajili wa shule za udereva nchini ili kupata wataalam wa fani waliopata mafunzo katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
DCP Kashai amewataka Wakuu wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini kusimamia vyema mifumo hiyo mipya ili kuleta tija na utendaji wakisasa kwa madereva wanatumia vyombo vya moto hapa nchini huku akiwataka wakuu hao kusimamia vyema matumizi ya VTS na speed radar ili kuzuia ajali hapa nchini.

Aidha,ametumia fursa hiyo kuwapongeza kwa namna walivyoendelea kudhibiti ajali kipindi cha mwisho wa mwaka na mwanzoni mwa mwaka 2024 huku akiwataka kuendelea kutoa elimu ya namna bora ya matumizi ya Barabara ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Kwa upande wake Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Pili Misungwi amesema, mfumo huo unakwenda kudhibiti madereva wasio na sifa ambapo amewaomba wakuu wa kikosi hicho kuyapokea mafunzo hayo ambayo yanakwenda kumaliza changamoto zilizokuwepo.

Mkuu wa Taasisi ya Mitambo Mizito na Teknolojia, Asia Nyuda Ntembo amesema, lengo la mfumo huo ni kuvitambua vyuo ambavyo vimesajiliwa ambao amebainisha kuwa waliona changamoto hiyo kitendo kilichopelekea kuungana na Jeshi la Polisi na kuja na mfumo wa Pamoja wa kuvitambua shule za udereva.
Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya Mitambo mizito na Teknolojia IHET, Naibu Kamishna wa Polisi mstaafu, Mohamed Mpinga amesema kuwa, hapo awali kulikuwa na changamoto huku akisema taasisi hiyo itasaidia kudhibiti shule za udereva zisizokuwa na sifa hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news