Sekta Binafsi ni mdau wa uchumi na maendeleo-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali inaiangalia sekta binafsi kwa mtazamo chanya wa kuwa mdau muhimu wa uchumi na maendeleo.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Februari 19,2024 alipofungua Mkutano mkuu wa kumi na tano(15) wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa tayari kazi ya kuandaa sheria inayohusisha maendeleo ya sekta binafsi inaendelea chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ikisimamiwa na Sekretarieti ya Baraza la Taifa la Biashara.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amemtaka Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe.Omar Said Shaaban kusimamia kukamilika kwa sheria hiyo mwishoni mwaka huu.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kuitangaza Zanzibar katika majukwaa mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa kuvutia wawekezaji wengi zaidi ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali imeanzisha mifumo mbalimbali ya kurahisisha mazingira bora ya kufanya biashara nchini katika kuendana sambamba na maendeleo ya dunia ya sayansi na teknolojia ili kurahisisha huduma za maisha ya wananchi.
Rais Dkt.Mwinyi pia ametoa wito kwa wafanyabiashara wote kufanya biashara kwa misingi ya haki na uadilifu kwa mujibu wa sheria ikiwemo kulipa kodi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news