Prof.Muhongo aipa mbinu Serikali uhakika wa chakula

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo ametoa mchango wake kuhusu usalama wa chakula nchini, biashara ya chakula duniani na kilimo cha umwagiliaji.

Aidha,ameshauri pawepo na mikakati madhubuti ya kuongeza uzalishaji hasa katika mazao ya mahindi, mchele, ngano kutokana na umuhimu wake kwa watu wengi zaidi hapa nchini na duniani.
Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine Prof. Muhongo amesema kuwa kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) mazao yanayotumika sana ni mchele, ngano, mahindi, viazi na sukari.

Vile vile amesema, asilimia 80 ya watu duniani ambao ni bilioni 8.1 chakula chao kikuu ni mchele, mahindi na ngano lakini bado uzalishaji si wa kiwango kikubwa.

Amesema kuwa, Tanzania inapaswa kwenda mbio na kujikita katika kilimo cha umwagiliaji na matumizi sahihi ya mbolea ili kuzalisha kwa kiwango kikubwa.

Prof. Muhongo amesema, yapo mataifa ikiwemo India na China ambayo kwa sasa yamepiga hatua katika Sekta ya Kilimo na kuiacha Tanzania nyuma licha ya kuwa karibu sawa miaka ya 1960.

"Tunahitaji umwagiliaji na kutumia mbolea, sehemu kubwa duniani mbolea wanayoitumia ni NPK...tuwekeze kwenye mahindi yanatumiwa na watu wengi.

"Pia mchele na ngano. Asilimia 50 ya wakazi wa Dunia hii wanatumia mchele, kwa sasa kilimo tulicho nacho ni biashara na pia tulime mpunga. Msimu uliopita walizalisha tani milioni 520 na mzalishaji wa kwanza ni China.

"Alizalisha karibu tani milioni 200 na wa pili India alizalisha tani karibu milioni 189, duniani bado ni wale wale tulikuwa karibu sawa miaka ya 1960 kwa sasa wanaongoza upande wa kilimo kwa nini tusijifunze kwao.

"Ngano asilimia 40 ya watu duniani wanatumia kama chakula kikuu, msimu uliopita zilizalishwa tani milioni 760.

"Bado ni China na wa pili India na wazalishaji sita bora ni India, China, Rusia, Marekani, Ufaransa na Canada,"amesema Prof.Muhongo.

Tafadhali msikilize Prof. Muhongo katika video hapa chini;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news