Rais Dkt.Mwinyi aifariji familia ya Lowassa

DAR ES SALAAM-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, amewahi kufanya kazi na Hayati Edward Ngoyai Lowassa kwa vipindi tofauti katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Awamu ya Tatu na Awamu ya Nne.
Amesema, taarifa ya msiba huo ameipokea kwa masikitiko makubwa, pia anatoa pole kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wote kwa ujumla.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Februari 12,2024 alipofika nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Lowassa, akiwa na Mama Mariam Mwinyi, kwa lengo la kuwafariji wanafamilia wa marehemu aikiwemo Mama Regina Lowassa, Masaki jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news