Rais Dkt.Samia aipongeza Yanga SC kwa kuichapa CR Belouizdad mabao 4-0

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vizuri katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Ni baada ya kuifunga CR Belouizdad mabao manne kwa sifuri na kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali.

Mtannge huo umepigwa Februari 24,2024 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

"Naipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vyema katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali.

"Mafanikio haya yameandika historia kubwa kwa klabu na sekta ya michezo nchini. Mmeleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki wenu na Watanzania kwa ujumla,"amesisitiza Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Mabao hayo manne yaliwekwa nyavuni na Mudathir Yahya Abbas dakika ya 43, Stephane Aziz Ki dakika ya 47.

Mengine yamefungwa na Kennedy Musonda dakika ya 48 na Joseph Guede Gnadou dakika ya 84 ya kipindi cha pili cha mchezo huo.

Chini ya Kocha Miguel Ángel Gamondi, kwa matokeo hayo Yanga inafikisha alama nane na kusogea nafasi ya pili ikiwa ni nyuma ya mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri baada ya wote kucheza mechi tano.

Aidha,CR Belouizdad wanabaki na alama zao tano mbele ya Medeama SC ya Ghana yenye alama nne inayoshika mkia baada ya wote kucheza mechi tano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news