Rais Dkt.Samia amedhamiria kumtua mama ndoo kichwani-Waziri Mkuu

NA FRESHA KINASA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kutekeleza kampeni yake ya kumtua ndoo mama kichwani,hivyo wananchi waendelee kumuamini na kumuunga mkono kwa dhati.
Hatua hiyo inalenga kuwezesha kila mtanzania kupata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao na kuwaondolea usumbufu wa kupata huduma ya maji safi na salama.

Waziri Mkuu Majaliwa amebainisha, Serikali ya Awamu ya Sita ipo imara na itaendelea kuwahudumia kwenye mambo yote ya msingi ambayo ni mahitaji ya kila siku ikiwemo afya, maji, barabara na elimu.

Amesema hayo leo Jumatano Februari 28, 2024 wakati alipokagua mradi wa maji wa Komuge uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Aidha,Mheshimiwa Majaliwa amewataka watumishi wa Halmashauri zote nchini kuwa na utaratibu wa kufanya ziara kwenye maeneo yao ili wasikilize changamoto za wananchi na kuzifanyia kazi.

Ameongeza kuwa, kuwajibika kwa viongozi wa ngazi mbalimbali katika maeneo yao kutaleta msukumo chanya na wa dhati wa kuleta maendeleo kwa Wananchi na kukidhi matakwa ya dhamira ya Serikali kutoa huduma bora kwa Wananchi wake.

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kuwa ndani ya wiki hii Shilingi milioni 720 zitatolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji Komuge ili ndani ya miezi mitatu uwe umekamilika” mhandisi wa maji mkoa na wilaya anzeni kusafisha eneo kwa ajili ya eneo ambalo litajengwa tenki."
Nao wananchi wa Komuge wakizungumza na DIRAMAKINI kando ya hadhara hiyo, wamemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kufanya ziara katika mradi huo hatua ambayo wamesema imesaidia kutolewa kwa fedha za utekelezaji wa mradi huo.

"Ujio wa Waziri Mkuu umeleta neema kwetu Wananchi, pesa zimetolewa ili mradi wetu utunifaishe Wananchi hasa kina mama ambao ndio walengwa wakubwa wa maji katika familia zetu,"amesema Rhoda Chacha.
Naye Esta Fabiani ameiambia DIRAMAKINI kuwa,upatikanaji wa Maji kwa wepesi utasaidia wananchi hasa kina mama kushiriki katika shughuli za maendeleo kwani watapata maji kwa uhakika na haraka. Huku akimshukuru Rais Dkt. Samia kwani katika uongozi wwke ameleta mageuzi makubwa kwa kuimarisha huduma ya maji maeneo mengi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news