Yanga SC kiboko yao

DAR ES SALAAM-Klabu ya Yanga (Young Africans Sports Club) ya jijini Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.
Ni katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa barani Afrika ambao umepigwa Februari 24,2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Mabao hayo yaliwekwa nyavuni na Mudathir Yahya Abbas dakika ya 43, Stephane Aziz Ki dakika ya 47.

Mengine yamefungwa na Kennedy Musonda dakika ya 48 na Joseph Guede Gnadou dakika ya 84 ya kipindi cha pili cha mchezo huo.

Chini ya Kocha Miguel Ángel Gamondi, kwa matokeo hayo Yanga inafikisha alama nane na kusogea nafasi ya pili ikiwa ni nyuma ya mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri baada ya wote kucheza mechi tano.

Mshairi wa kisasa,Dkt. Mohamed Omary Maguo anakuletea utenzi wa kuipongeza timu ya Yanga kwa ushindi kwa kishindo wa magoli manne kwa sifuri dhidi ya timu ya Beluzdadi ya Algeria katika hatua ya makundi ya klabu Bingwa ya Afrika.

Ushindi huu mnono umeiwezesha Yanga kuingia hatua ya Robo fainali na kuendelea kuliletea heshima taifa letu la Tanzania. Endelea;

1.Amedundwa kama ngoma
Kisiki cha mchongoma
Beluzdadi kakoma
Kabaki ameduwaa

2.Kabaki ameduwaa
Magoli yakamjaa
Dakika mbili waaa
La Tatu likaingia

3.Akiwa bado anang'aa
Macho akishangaaa
Mara chwaaaaaa
La Nne kalivagaa

4.Kama vile mshumaa
Wamulika ki'ambaa
Yanga katia ngaaa
Beluzi kabaki ngoo

5.Pira lile biriani
Kachumbari pilauni
Maragwe chapatini
Yanga ya kimataifa

6.Mishikaki lo' laini
Firigisi na maini
Kila mtu atamani
Pira lile lao Yanga

7.Amekubali mtani
Kwamba Yanga ni sukani
Pira lile uwanjani
Jamani Yanga ni moto

8.Jamani Yanga ni moto
Weka mbali na watoto
Pacome kwa mkong'oto
Beluzi tasimulia

9.Blichi kama kokoto
Kizubaa wala ngoto
Kigeukia kushoto
Kulia wapigwa Nne

10.Beluzi mwenye majuto
Ameulamba msoto
Wa kikubwa si kitoto
Yanga ndiyo bingwa

11.Yanga yetu ya heshima
Mbele sijerudi nyuma
Robo umeshaipima
Nusu na final hiyoo

Karibuni sana Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa sasa tunapokea maombi ya Muhula wa Aprili 2024 katika ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada. 

Pia tunapokea maombi ya Stashahada za Uzamili, shahada za Umahiri na Uzamivu duru ya Tatu. Tuma maombi yako kupitia www.out.ac.tz ukiwa mahali popote pale.

MTUNZI

Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mshairi wa Kisasa
Mhadhiri Mwandamizi
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

28/02/2024

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news