Rais Dkt.Mwinyi ateta na ujumbe kutoka Canada,Afrika

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Kyle Nunas na ujumbe wa Wenyeviti wa Jumuiya ya Mabunge ya Canada na Afrika wakiongozwa na Seneta, Amina Gerba katika Ikulu ya Zanzibar leo Februari 22,2024.
Rais Dkt.Mwinyi amesema, sekta kuu ya uchumi wa Zanzibar ni utalii ambao unachangia asilimia 30 ya pato la Taifa, pia ameikaribisha Canada kuangalia fursa zilizopo katika uchumi wa buluu ikiwemo utalii, uvuvi, usafiri wa vyombo vya baharini, bandari , mafuta na gesi.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Serikali ya Canada kwa ushirikiano wa miradi mbalimbali ya huduma za kijamii ikiwemo elimu na afya.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amesema, Muungano wa Tanzania ni wa kipekee utaendelea kuwa mfano wa kuigwa Afrika.

Pia katika mazungumzo hayo amegusia suala la uhuru wa habari, Serikali ya umoja wa kitaifa, nafasi za uwakilishi kwa Wanawake, uwekezaji pamoja na nishati hususani umeme.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news