Mwenyekiti CCM Mkoa wa Tabora,Hassan Wakasuvi afariki

TABORA-Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi ambaye pia alikuwa Mlezi wa chama wa Mkoa wa Arusha amefariki dunia.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa Balozi, Dkt.Batilda Burian amethibitisha kutokea kifo hicho na kubainisha kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuondokewa na Kiongozi wao.

Amesema kuwa, marehemu Wakasuvi amepatwa na umauti huo baada ya kuanguka akiwa ofisini kwake ambapo viongozi na WanaCCM waliokuwepo ofisini hapo walimkimbiza Hispitali ya Rufaa ya Mkoa huo, Kitete kwa ajili ya matibabu zaidi,lakini haikusaidia kuokoa maisha yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news