REA ni kama injini ya maendeleo vijijini


Kupitia umeme wa REA ambao umesambaa vijiji vingi hapa nchini, makundi mbalimbali ya wanajamii wakiwemo vijana wa kike kwa kiume wamejiajiri kupitia shughuli zinazotumia nishati ya umeme nchini. (Picha na michaelngilangwa).

"Pongezi kwa REA kwa kazi kubwa sana waliyofanya. Sisi tumekuja kuongeza nguvu. Tunajua Serikali ina mikakati ya kuwaletea maendeleo watu wake na REA ni taasisi muhimu sana katika kuleta maendeleo vijijini. Ni kama Injini ya maendeleo vijijini.
"Tutachukua yale mazuri na kuyaboresha zaidi. Bodi zilizopita zimefanya kazi nzuri sana. Tutaanzia walipoishia na kuendelea.
 
"Tutajitahidi kutumia nguvu zetu zote na Mungu atusaidie ili tuweze kufanya kazi nzuri katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwa ajili ya wananchi wetu vijijini,"Stephen Mwakifamba, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini - Feb. 2024.
"Jukumu letu liko wazi maana tunatakiwa kuangalia zaidi na kupeleka huduma za nishati bora vijijini kwa kuzingatia miongozo iliyopo. Kuna Mpango Mkakati wa REA wa miaka mitano, lakini pia kuna Mpango Kazi ambao unaendelea kutekelezwa sasa hivi. 

"Kupitia hiyo, kama Mjumbe wa Bodi, nimejipanga kuwa ninaenda kutoa mchango wangu ili kutimiza azma ya Serikali ya kuweza kufikia malengo ya Watanzania wote kupata nishati bora,"Florian Haule,Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini - Feb. 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news