Serikali yataja faida za mfumo wa ufundishaji mubashara

DODOMA-Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt.Charles Msonde amesema, mfumo wa ufundishaji mubashara ulioko Dodoma Sekondari na Kibaha ni wa majaribio ambao umefanywa kutokana na ushauri na maelekezo ya wabunge katika kuboresha elimu na kutumia teknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji katika kupunguza changamoto ya upungufu wa walimu.
“Kwa sasa serikali imepeleka baadhi ya vijana kwenda kusoma zaidi nchini China na hii unayoona ni mpenda maendeleo Eduteck ameiona atusaidie kufanya majaribio kwa kutusaidia madarasa janja manne moja likifungwa Zanzibar, Kibaha, Shule ya Sekondari Iyumbu na Taasisi ya Elimu Tanzania.

“Pia Huwawei amesaidia kujenga madarasa janja mawili ambapo moja liko Shule ya Sekondari Dodoma na Shule ya Sekondari Kibaha na madarasa haya janja si tu yatatumiwa na wanafunzi bali pia yatatumika kufanya kufundisha walimu kazini katika maeneo mbalimbali nchini.”

Naye Mkurugenzi Huduma za Elimu kutoka Shirika la Elimu Kibaha, Dk Rogers Shemwelekwa alisema Tanzania ni ya kwanza barani Afrika kwa kutumia mfumo wa ufundishaji mubashara na kuwa Ivory Coast na Afrika Kusini wao wanatumia mfumo wa ufundishaji kidijitali na si ufundishaji mubashara.

“Hili ni jambo kubwa katika mapinduzi ya elimu, kwa Afrika Tanzania ni ya kwanza, kuna nchi kama Ivory Coast na Afrika kusini wao wana online teaching (ufundishaji kidijitali) na sio live teaching ambayo ni very interactive (ushirikiwa moja kwa moja).”

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Dodoma, Faith Shinzeh alisema mfumo umekuwa na manufaa kwao katika eneo la ujifunzaji kwasababu wamekuwa na ushirikiano na wenzao wa Shule ya Sekondari ya Kibaha kwasababu inatoa fursa ya kubadilishana maarifa na hivyo uelewa wetu unakua zaidi.

“Pia unatusaidia kujifunza kwa vitendo hali ambayo inafanya kuweza kukumbuka, mfano leo tumesemo fizikia mada ya energy transformation wakati wa mtihani kama sitakumbuka yote lakini videno inaweza kunikumbusha na na nitaweza kujibu. Pia inaongeza hari ya wanafunzi kusoma tukiwa na zamu ya kuja digital classroom kila mtu hataki kukosa.”

Naye mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kibaha, Gift Kabulunge alisema: “naishukuru sana Serikali kwa kuwawekea mfumo huo mpya ambao umenisaidia masomo yote niliyoshiriki kuyaelewa nakubaki kwenye jumbukumbu zangu. Pia umetuongezea hari ya kujifunza na kubadili nyanya ya kielimu.

“Kabla ya mfumo huu walimu walikuwawanatufundisha kwa njia ya ubao, hii inatufanya wanafunzi tuwe tuna imagination (kufikirika) kile mwalimu anachotufundisha, lakini kwa mfumo huu unaoana kitu anachofundisha kwa uhalisia wake.”

Pia Gift aliomba Serikali kuharakisha mfumohuo kufika shule nyingine hii itasaiaida kuongeza wigo wao wa kujifunza na kuongeza ufaulu na kuweza kusaidia maendeleo ya nchi yetu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news