Utii wa Sheria ya Matumizi Salama ya Mionzi mikoa ya Mwanza na Geita waongezeka

GEITA/MWANZA-Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) imeridhishwa na utii wa sheria ya matumizi salama ya mionzi katika zoezi la ukaguzi unaoendelea kwenye vituo vinavyotumia mionzi katika mikoa ya Mwanza na Geita.
Zoezi hili maalumu ambalo hufanyika kila mwaka mara moja ni la kawaida na hufanyika mahususi nchini kote katika kuhakikisha matumizi ya mionzi katika vituo vinayotumia mionzi katika sekta mbalimbali.

Miongoni mwa sekta hizo ni kama vile afya, migodi, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli na viwanda.
Lengo ni kuhakikisha unazingatia sheria, kanuni na taratibu za matumzi salama ya mionzi ili kulinda mazingira, wagonjwa na wafanyakazi wanaotumia vyanzo vya mionzi katika kazi zao za kila siku pamoja na wananchi wote dhidi ya madhara yatokanayo na mionzi.

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita baada ya kufanya zoezi la ukaguzi, Mkaguzi Mwandamizi wa mionzi wa TAEC, Bw. Jerome Mwimanzi amesema,ukaguzi huo ni muhimu ili kujiridhisha kama mashine zinafanya kazi vizuri.
Pia, majengo hayavujishi mionzi na watumiaji wanafuata sheria, kanuni na taratibu za matumizi salama ya mionzi.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Dkt. Mfaume Salim Kibwana amesema, anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa wa mashine za uchunguzi kwa kutumia mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.
Naye Mtekinolojia wa mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Yohana Sospeter amesema,ukaguzi wa TAEC unawasaidia katika kuhakikisha utoaji wa huduma ya mionzi inakuwa salama kwa wagonjwa wanaowahudumia.

Sambamba na kujilinda wao kama watoa huduma dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi.

Katika ukaguzi uliofanyika mkoani Mwanza jumla ya vituo 48 vimekaguliwa zikiwemo hospitali, viwanda, uwanja wa ndege, ujenzi wa reli ya SGR Pamoja na Daraja la Kigongo Busisi.
Aidha,kati ya hivyo vituo vinne sawa na asilimia 8 vimefungiwa kutoa huduma hadi hapo vitakapokidhi matakwa ya sheria na kanuni za kumiliki na kutumia vyanzo vya mionzi.

Ambapo vituo 44 vilivyokidhi matakwa ya kisheria na kuruhusiwa kuendelea kutoa huduma ni sawa na asilimia 92.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news