Ujio wa Waziri Mkuu ni neema kwetu, Musoma Vijijini tumlaki kwa wingi-Prof.Muhongo



NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo amewaomba wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kuhudhuria kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anaendelea na ziara ya kiserikali mkoani Mara kuanzia Februari 25, 2024 hadi Februari 29, 2024. Ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma atafanya ziara siku ya Februari 29,2024.

Huku Mbunge wa Jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo na wananchi wakiwa wamejiandaa vyema kumpokea kwa shangwe na vifijo.

Akiwa katika Jimbo la Musoma Vijijini, Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo kijijini Suguti na kufanya kikao cha ndani cha madiwani na wafanyakazi wa halmashauri hiyo.

Aidha, tukio la pili atakalofanya Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa akiwa katika halmashauri hiyo ni kufanya mkutano wa hadhara kijijini Bwai Kumsoma ambapo atazungumza na wananchi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini tarehe 26 Februari, 2024 imesema "Tunaendelea kujitayarisha. Ng'ombe wawili wameshafikishwa kijijini Bwai Kwitururu,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news