Ujumbe wa NDC watembelea Wizara ya Mambo ya Nje

DODOMA-Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) amekutana na Ujumbe wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) jijini Dodoma, Februari 19, 2024.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Mej. Gen. Wilbert Ibuge akitoa zawadi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo baada ya ujumbe wa chuo hicho kufanya ziara ya mafunzo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma.

Ujumbe huo unaongozwa na Mkuu wa Chuo cha NDC, Balozi Meja Jenerali Wilbert A. Ibuge, upo katika ziara ya mafunzo ya kutembelea taasisi mbalimbali kujifunza kuhusu mchango wa taasisi hizo katika maendeleo ya nchi hususan kwenye sekta ya ulinzi. Ujumbe huo wenye jumla ya washiriki 88, unahusisha Wakufunzi 33, na Wanachuo 55 kutoka Tanzania na mataifa ya Afrika ikiwemo Nigeria, Namibia, Misri, Zambia na Zimbabwe.

Mej. Gen. Ibuge alieleza kuwa malengo ya chuo hicho ni kuwandaa Maafisa Waandamizi ndani na nje ya nchi kutoka vyombo vya Usalama na Watumishi wa Umma katika nyanja ya Usalama na Stratejia. Wakati wa ziara hiyo, ujumbe huo umeshiriki kwenye mjadala kuhusu Umuhimu wa Kuimarisha usalama wa jamii zinazoishi mipakani kwa ajili ya usalama endelevu wa Taifa (Enhancing Border Community Security for Sustainable National Security).
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Mej. Gen. Wilbert Ibuge wakati ujumbe wa chuo hicho ulipofanya ziara ya mafunzo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Chiku Kiguhe akitoa neno la ukaribisho wakati wa kikao baina ya uongozi wa Wizara na ujumbe kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akitoa neno kuhusu majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, hususan yanayohusu ulinzi na usalama kwa wanachuo wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Mej. Gen. Wilbert Ibuge akitoa maelezo mafupi kuhusu malengo na majukumu ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi wakati wa kikao baina ya uongozi wa Wizara na ujumbe wa chuo hicho.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akitoa neno kuhusu majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, hususan yanayohusu ulinzi na usalama kwa wanachuo wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Haji Janab akitoa wasilisho kuhusu majukumu ya Wizara wkati wa kikao baina ya uongozi wa Wizara na ujumbe wa chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Mej. Gen. Wilbert Ibuge akitoa maelezo mafupi kuhusu malengo na majukumu ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi wakati wa kikao baina ya uongozi wa Wizara na ujumbe wa chuo hicho.
Mmoja wa wanachuo wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi akijitambullisha wakati ujumbe wa chuo hicho ulipofanya ziara ya mafunzo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma.
Mwanachuo akijitambulisha.
Mwanachuo akijitambulisha.
Mwanachuo akijitambulisha.
Mwanachuo akiuliza swali baada ya kusikiliza wasilisho kuhusu majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mwanachuo akiuliza swali baada ya kusikiliza wasilisho kuhusu majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Ujumbe huo umepokea wasilisho kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambapo Balozi Dkt. Shelukindo alielezea majukumu ya Wizara hususan katika kuhamasisha usalama mipakani.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akijibu maswali mbalimbali yayoulizwa na wanachuo wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Mej. Gen. Wilbert Ibuge akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa kikao baina ya uongozi wa Wizara na ujumbe kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi.

Majukumu hayo yanahusisha uratibu wa mikutano ya ujirani mwema na Tume za Kudumu za Pamoja za Ushirikiano (JPCs), Vituo Vya Utoaji Huduma Kwa Pamoja Mipakani (OSBPs), na kuratibu itifaki za kikanda na kimataifa.
Mwanachuo akiuliza swali baada ya kusikiliza wasilisho kuhusu majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Mhandisi Abdillah Mataka akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Vituo vya Pamoja vya Mipakani.
Mwakilishi kutoka Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Amani Mwatonoka akifafanua masuala ya usalama katika mipaka wakati wa kikao baina ya kikao baina ya uongozi wa Wizara na ujumbe wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Mwanachuo akitoa neno la hukrani baada ya kikao baina ya kikao baina ya uongozi wa Wizara na ujumbe wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akitoa zawadi kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Mej. Gen. Wilbert Ibuge baada ya ujumbe wa chuo hicho kufanya ziara ya mafunzo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma.

Aidha, Wizara na Chuo cha NDC zimeahidi kuendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali yakiwemo mafunzo kwa Watumishi na maeneo mengine muhimu kwa maslahi ya pande zote mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news