Uzalishaji maji Ruvu Chini warejea katika hali ya kawaida

PWANI-Kazi ya marekebisho ya pampu ya kusukuma maji katika mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini imekamilika.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salam (DAWASA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,marekebisho hayo yalipelekea upungufu wa uzalishaji maji kutoka lita milioni 270 hadi lita milioni 220 kwa siku.

"Matengenezo yamekamilika leo Februari 25, 2024 na kurudisha hali ya uzalishaji katika kawaida yake ya ujazo wa lita milioni 270 kwa siku."

Aidha,maeneo yafuatayo yataanza kupata huduma ya maji kwa msukumo mzuri ikiwemo Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe,

Lugalo, Makongo, Chuo, Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni,

Mengine ni Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na katikati ya Jiji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news