Tanzania kupeleka Kili Marathon duniani

KILIMANJARO-Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuzifanya mbio za Kili Marathon kuwa bora zaidi duniani.

Ni kutokana na ubora ulioonekana kuoneshwa na wakimbiaji wa mbio hizo katika bara la Afrika kupitia Tanzania.
Hayo yamesemwa Februari 25, 2024 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliposhiriki mbio hizo za msimu wa 22 Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amewapongeza waandaji wa mbio hizo kwa kuzifanya kuwa za Afrika.

Mhe. Ndumbaro amesema kuwa, azma ya kuzipeleka mbio hizo duniani inawezekana kutokana na uwepo wa vivutio vingi vya utalii ambavyo vinavuta watu wengi kuja nchini.

Aidha, Mhe. Ndumbaro amezitangaza mbio hizo kuwa, kuanzia sasa zitakua ni mbio mama kwa mbio zote nchini kutokana na kusababisha kuwepo kwa mbio nyingine nyingi zinazofanyika nchini.

Mbio za Kili Marathon mwaka huu zimehusisha wakimbiaji kutoka nchi 56 duniani ikiwemo Marekani, Uingereza, Uholanzi, Ufaransa Kenya, Uganda na Afrika Kusini kwa wakimbiaji wa umbali wa KM 42, KM 21, na KM 5.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news