Watu 25 wafariki ajali ya Arusha

NA ABEL PAUL
Tanpol

WATU 25 wameafariki dunia huku wengine 21 wakijeruhiwa katika ajali iliyotokea maeneo ya Ngaramtoni kibaoni by Pass ikihusisha Lori na magari mengine madogo matatu Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Akitoa taarifa ya ajali hiyo Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi  CP Awadhi Juma Haji alipofika katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru amesema ajali hiyo ilitokea Februari 24,2024 muda wa saa 11:00 jioni.

Ni katika Barabara ya Arusha Namanga ambapo ilihusisha lori lenye namba za usajili KAC 943 H aina ya Mack lenye tela namba za usajili ZF 6778 mali ya kampuni ya KAY Construction ya Nairobi Nchini Kenya.

CP Awadhi ametaja idadi ya waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni wanaume (14) wanawake (10) na mtoto mmoja wa kike ambao jumla yao ni (25) huku akiitaja idadi ya raia wa kigeni waliofariki kuwa ni saba (07).

Katika ajali hiyo pia CP Awadhi ametaja idadi ya majeruhi kuwa ni 21 kati yao wanaume ni kumi na nne (14) na wanawake ni saba (07).

Ametaja magari yaliyopata ajali katika tukio hilo kuwa ni T 623 CQF aina ya Nissan Caravan, T 879 DBY aina ya Mercedes Benz Saloon na gari namba T 673 DEW aina ya Toyota coaster mali ya shule ya (New Vision School).

Pia Kamishna huyo wa opereshini na mafunzo ya Jeshi la Polisi nchini amekitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa kuwa ni kufeli breki ya lori kitendo kilichopelekea lori hilo kuyagonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake.

Amebainisha kuwa, Jeshi hilo linaendelea kumtafuta dereva aliyesababisha ajali hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Sambamba na hilo ametoa pole kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla na raia wa kigeni waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news