Waziri Dkt.Nchemba aishukuru IMF kwa kusaidia maendeleo ya nchi

NA BENNY MWAIPAJA

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa ajili ya kuchachua na kutengemaza uchumi kupitia sekta za uzalishaji.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa 7 kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, ikiongozwa na Bw. Harris Charambos Tsangarides (wa 7 kushoto), baada ya kufungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa ajili ya kuchachua na kutengemaza uchumi kupitia sekta za uzalishaji, Jijini Dodoma.

Alitumia fursa hiyo kulishukuru Shirika hilo kwa kutoa fedha zinazotumika kutekeleza miradi inayosaidia kuchochea maendeleo ya wananchi, kukuza uchumi jumuishi na kuiwezesha nchi kuhimili misukosuko ya kiuchumi inayoikabili dunia.

Dkt. Nchemba alisema kuwa kiasi cha takriban shilingi trilioni 1.3 kilichotolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya uviko 19 na kiasi kingine cha shilingi trilioni 2.8 kitakachotolewa na IMF kwa awamu saba kwa miaka mitatu kuanzia mwaka wa Fedha 2022/2023 hadi mwaka wa fedha 2024/2025, kimeendelea kuchochea ukuaji wa uchumi na huduma za kijamii katika sekta za afya, maji, kilimo, ujenzi wa miundombinu, uboreshaji wa mazingira ya kufanyia biashara.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akifungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa ajili ya kuchachua na kutengemaza uchumi kupitia sekta za uzalishaji, Jijini Dodoma.

“Tunaishukuru Bodi ya Wakurugenzi ya IMF kwa kuidhinisha tathimini ya awamu ya pili ya ECF mwezi Desemba mwaka 2023 na kutoa kiasi cha dola za Marekani 150.5 milioni na kufanya nchi ipokee jumla ya dola za Marekani 455.3 milioni za mpango wa ECF kwa awamu mbili hadi sasa,”alisema Dkt. Nchemba.

Alitumia pia nafasi hiyo kuiomba IMF, kuisaidia Serikali kupata fedha kupitia dirisha lake la Resilient and Sustainable Trust (RST), kwa ajili ya kusaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, Bw. Harris Charambos Tsangarides (kulia), akizungumza jambo wakati Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipofungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa ajili ya kuchachua na kutengemaza uchumi kupitia sekta za uzalishaji, jijini Dodoma. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini Tanzania,Bw. Sebastian Acevedo.

“Mimi na timu yangu tupo tayari kwa mazungumzo na kuweka malengo yanayopaswa kutimizwa ndani ya muda ambao tutakuwa tumeshauriana ili kuweza kutekeleza program ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,”alisema Dkt. Nchemba.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akipeana mkono na Mshauri wa Idara ya Afrika kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Harris Charambos Tsangarides, baada ya kufungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa ajili ya kuchachua na kutengemaza uchumi kupitia sekta za uzalishaji.

Kwa upande wake Kiongozi wa Timu hiyo ya IMF Bw. Harris Charambos Tsangarides, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutekeleza kwa umahili mpango wa ECF na kutimiza vigezo vilivyoweka katika mpango huo kwa wakati na kusaidia nchi kupata kiasi cha dola za Marekani 150.5 mwezi Desemba mwaka 2023.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akimsikiliza Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, Bw. Harris Charambos Tsangarides, wakati wa kufungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam hao) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa ajili ya kuchachua na kutengemaza uchumi kupitia sekta za uzalishaji, Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha-Dodoma).

Akijibu maombi ya Mhe. Waziri wa Fedha kuhusu upatikaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Bw. Tsangarides, alisema kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kupata fedha hizo na kushauri kukamilisha maandalizi ya awali kwa wakati ikiwemo tathimini ya sera za nchi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuingia katika majadiliano na IMF mwezi Aprili 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news