Waziri Dkt.Nchemba akutana na wataalamu wa Tathmini ya Uchumi kutoka SADC


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiongoza kikao kati yake na timu ya watalaam wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walioongozwa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi kutoka Benki ya Zimbabwe, Bw. Nebson Mupunga, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akieleza kuhusu juhudi za Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi ili kuwa na Uchumi imara, wakati wa mkutano na timu ya watalaam wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walioongozwa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi kutoka Benki ya Zimbabwe, Bw. Nebson Mupunga (hayupo pichani), jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa timu ya watalaam wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi kutoka Benki ya Zimbabwe, Bw. Nebson Mupunga, akizungumza jambo wakati wa mkutano na wataalamu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Idara ya Usimamizi wa Madeni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Lekinyi Mollel, akizungumza jambo wakati wa mkutano kati yake na timu ya watalaam wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), waliofika kutathmini maendeleo ya Uchumi, jijini Dar es Salaam.
Timu ya watalaam wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walioongozwa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi kutoka Benki ya Zimbabwe, Bw. Nebson Mupunga (wa sita kulia), ikiwa katika mkutano na wataalamu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati wa tathmini ya Uchumi wa Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Timu ya watalaam wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walioongozwa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi kutoka Benki ya Zimbabwe, Bw. Nebson Mupunga (wan ne kushoto), ikiwa katika mkutano na wataalamu wa Economic and Social Research Foundation (ESRF), wakati wa tathmini ya Uchumi wa Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Idara ya Usimamizi wa Madeni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Lekinyi Mollel (wa pili kushoto) na timu ya watalaam wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walioongozwa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi kutoka Benki ya Zimbabwe, Bw. Nebson Mupunga (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka SADC na BoT, jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news