Waziri Mkuu awasili Tabora kushiriki maziko ya Wakasuvi


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Tabora ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa katika maziko ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Hassan Wakasuvi.
Wakasuvi ambaye pia alikuwa Mlezi wa chama wa Mkoa wa Arusha alifariki dunia Februari 22,2024.
Alipatwa na umauti huo baada ya kuanguka akiwa ofisini kwake ambapo viongozi na WanaCCM waliokuwepo ofisini hapo walimkimbiza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo, Kitete kwa ajili ya matibabu zaidi,lakini haikusaidia kuokoa maisha yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news